Press Clipping
11/05/2018
Article
BOOMPLAY, UNIVERSAL MUSIC GROUP WATANGAZA USHIRIKIANO KATIKA USAMBAZAJI MUZIKI

LAGOS NA SANTA MONICA, 5 Novemba 2018 – Boomplay, huduma ya muziki inayoongoza upande wa kusikiliza na kupakua muziki na Universal Music Group (UMG), kampuni inayoongoza katika usambazaji wa muziki ulimwenguni, leo wanatangaza kusainiwa kwa makubaliano ya kibali cha kusambaza muziki katika masoko mengi ndani ya Afrika.

UMG ni kampuni ya kwanza ya muziki wa kupitisha leseni yake kwa Boomplay, ambayo inajulikana kwa huduma yake ya kusikiliza muziki barani Afrika. Chini ya makubaliano ya mkataba huu wa miaka mingi na ufanisi mara moja, Boomplay itasambaza muziki kutoka kwa UMG nchini Tanzania pamoja na Nigeria, Ghana, Kenya, Rwanda, Uganda na Zambia. Mpaka sasa, Boomplay ina nyimbo zaidi ya milioni mbili na maelfu ya video zinazopatikana kwa watumiaji wake zaidi ya milioni 36, na watumiaji karibu milioni mbili wanaoongezeka kila mwezi.

Watumiaji wa Boomplay sasa wanaweza kupata nyimbo za nyumbani na za kimataifa kutoka UMG wakiwemo wasanii kama Eminem, Tekno, Post Malone, Nicki Minaj, Lady Zamar, Lil Wayne, Bob Marley, Brenda Fassie, Wurld, J.Cole, Dr. Tumi, Nasty C, 6lack, Diana Ross, Hugh Masekela, Jon Bellion, Larry Gaaga, Tamia, Maroon 5, Aka & Anatii, TJAN, Jah Prayzah, Nonso Bassey, Mafikizolo, Cina Soul, Ella Mai, Mr. Eazi na wengine wengi.

Mapema mwaka huu, UMG ilitangaza uzinduzi wa Universal Music Nigeria, ikiwa na lengo la kuwapa wasanii fursa nyingi barani Afrika kwa ajili ya kufanikisha kazi zao kufika hatua za kimataifa. UMG inaendelea kusukuma gurudumu la lengo lao la kukuza mazingira ya muziki wa Afrika pamoja na kurekodi muziki, kuchapisha muziki, uzalishaji, matamasha, ushirikiano wa makampuni na jitihada za biashara.

Katika hili, Makamu wa Rais wa Universal Music Group, idara ya Maendeleo ya Masoko, Adam Granite alisema, “Tunatarajia kufanya kazi na Boomplay ambapo tutawawezesha wasanii wetu wa Kiafrika kuwa wabunifu, jukwaa la masoko na uendelezaji wa rasilimali ili kuharakisha kazi zao zinaendelea kukua barani Afrika. Mkataba huu utasaidia wasanii wa UMG kufikia watumiaji wapya, huku wakiongeza hamasa ya usikilizaji wa muziki wa Afrika ili watapate faida kuwafikia mashabiki wa muziki, wasanii wengine na wazalishaji muziki.

“Ushirikiano huu utaendelea kufikia watu wengi na kuhakikisha kazi za wasanii wetu zinawafikia mamilioni ya wapenzi wa muziki barani Afrika,” alisema Ezegozie Eze Jr., Meneja Mkuu wa Universal Music Nigeria, “Tunafurahia kuwa kampuni ya kwanza ya muziki kushirikiana na Boomplay na tunatarajia kuleta ubunifu wa hali ya juu kwa wasanii wetu na kwa watumiaji wengi Afrika. ”

Akizungumza pia, Mkurugenzi Mtendaji wa Boomplay, Joe He, alisema kuwa Boomplay itaendelea kuunda ushirikiano unaoimarisha mfumo wa kidigitali na kuunganisha wapenzi wa muziki na nyimbo wananazozipenda wakati wowote na mahali popote.

“Boomplay imejizatiti kuendelea kutengeneza shauku kubwa ya muziki wa kiafrika katika njia halali, hasa kwa watumiaji wa Boomplay kushirikiana na lebo kubwa za muziki duniani kama Universal Music Group inatoa nafasi nyingine kubwa kwa sisi kufanya hivyo “,
alisema.

App ya Boomplay ambayo kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa simu za Android, inatarajia kuzindua app kwenye jukwaa la iOS hivi karibuni. Kwa kuongeza, watumiaji wapya wa Boomplay wataweza kupata usajili wa miezi moja bila malipo pale watakapojiunga na kifurushi cha mwezi mmoja kinachojirudia.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na


Universal Music Group:

James Murtagh-Hopkins / +44 203 932 6822 james.murtagh-hopkins@umusic.com

Boomplay:

Tosin Sorinola / +234 8166896617 tosin.sorinola@transsnet.com

Natasha Stambuli / +255 677007428 natasha.stambuli@transsnet.com

Kuhusu Boomplay

Boomplay ni app inayotoa uwezo wa kusikiliza na kupakua nyimbo, inayomilikiwa na kampuni ya Transsnet Music Limited. App hii ina mamilioni ya nyimbo na video, ikiwaunganisha mashabiki wa muziki na nyimbo wazipendazo muda wowote. Mpaka sasa, Boomplay ina watumiaji zaidi ya milioni 32, kati yao zaidi ya milioni 10 ni kutoka Google Play Store na wengine ni watumiaji wa simu za TECNO, Infinix na itel. Huduma hii inapatikana katika mtandao na hasa kwenye mfumo wa Android. App hii ambayo imewahi kushinda tuzo ya “Best African App” katika tuzo za “Apps Africa” mwaka 2017, inawezesha watumiaji wake kusikiliza na kupakua nyimbo pamoja na kujiunga na kifurushi kitakachokuwezesha ku-save nyimbo na kusikiliza bila kutumia data. Kwa muda mrefu sasa, huduma nyingi za malipo zimeanzishwa na hili limewarahisishia mashabiki wa muziki kulipia nyimbo kupitia huduma za pesa kwa njia ya simu, benki pamoja na kadi za Boomcoin. Lengo kubwa la Boomplay ni kujenga mfumo endelevu kwenye tasnia ya muziki. Bofya hapa kujua zaidi.


Kuhusu Universal Music Group

Ni kundi la kimataifa linaloongoza katika burudani, usambazaji wa kazi za muziki, kurekodi muziki, kuuza kazi za muziki na video katika nchi zaidi ya 60 duniani. Ikiwa na orodha ya kina kwenye kurekodi nyimbo za kila ladha,UMG hutambulisha na kuendeleza wasanii pamoja na kusambaza muziki uliopendekezwa sana kibiashara. Ikiwa imejikita kisanaa, ubunifu na ujasiriamali UMG inakuza maendeleo ya huduma, majukwaa na mifano ya biashara ili kuongeza fursa za kisanii na kibiashara kwa wasanii wa Afrika na kujenga uzoefu wa huduma mpya kwa mashabiki. Universal Music Group ni kampuni ya Vivendi. Pata maelezo zaidi hapa.